KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, December 18, 2010

Steve Kean AJINADI KUITAKA KAZI YA UMENEJA ROVERS.


Meneja wa muda wa klabu ya Blackburn Rovers Steve Kean ameonyesha kuitamani nafasi ya aliekua bosi wake Sam Allardyce ambae mwanzoni mwa juma hili alitimuliwa huko Ewood Park.

Steve Kean ameonyesha kuitamani nafasi hiyo baada ya kukiri wazi kwamba yu tayari kwa jukumu hilo endfapo wamiliki wa Rovers wataamua kumpa nafasi ya umeneja klabuni hapo.

Amesema binafsi anajiona anafaa kuwa meneja wa Blackburn Rovers kufuatia vigezo alivyo navyo ambapo kubwa analojivunia ni kukaa kwa muda mrefui klabuni hapo akiwa kama meneja msaidizi.

Amesema anatambua mazingira mengi ya klabu hiyo hivyo litakua jambo zuri na la msimngi endapo wamiliki wa klabu hiyo wataamua kumpa nafasi ya Big Sam ambae hatua ya kuondoka kwake iliwashangaza wengi.

Hata hivyo amebainisha wazi kwamba anaamini huenda nafasi hiyo ikaangukia kwake endapo atafanya vyema katika michezo kadhaa ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza, hivyo ameahidi kuonyesha jitihada zake kwa lengo la kufikia mikakati aliyojiwekea.

Steve Kean hii leo ameanza kazi rasmi akiwa kama meneja wa muda ambapo amekishuhudia kikosi chake kikicheza nyumbani dhidi ya West Ham Utd.

No comments:

Post a Comment