KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, December 22, 2010

Howard Webb AHITAJI USAIDIZI WA UWANJANI.


Mmoja wa waamuzi maarufu duniani ametangaza kuiunga mkono sheria ya kutumika kwa kifaa maalum kitakachowawezesha waamuzi kutambua mpira umevuka mstari wa goli kwa lengo la kumaliza utata uliopo katika michezo kadhaa ya soka inayoendelea hivi sasa kwenye viwanja mbali mbali.

Muamuzi huyo maarufu duniani ni yule alifanikiwa kuchezesha fainali ya ligi ya mabingwa barani ulaya msimu uliopita kati ya Inter Milan dhidi ya Bayern Munich sambamba na mchezo wa hatua ya fainali ya kombe la dunia kati ya timu ya taifa ya Hispania dhidi ya timu ya taifa ya Uholanzi Howard Webb.

Akizungumza katika mahojiano maalum na shirika la utangazaji la nchini Uingereza BBC, Howard Webb amesema umewadiwa wakati kwa shirikisho la soka ulimwenguni FIFA kutambulisha sheria hiyo ambayo ana imani kubwa itamaliza mzozo unaowatia lawamani waamuzi wengi duniani.

Muamuzi huyo wa kimataifa toka nchini Uingereza, amesema wao kama waamuzi wanatakiwa kutoa maamuzi sahihi pasipo kumpendelea yoyote yule wanapokua uwanjani hivyo sheria hiyo itawasaidia kwa kufanya kazi yao kwa usahihi mkubwa.

Howard Webb ameomba kutambulishwa kwa sheria hiyo huku akikumbushia bao la utata lililofungwa na kiungo wa kimataifa toka nchini Uingereza Frank Lampard kwenye fainali za kombe la dunia za mwaka 2010 katika mchezo wa hatua ya robo fainali kati ya Uingereza dhidi ya Ujerumani.

Amesema utaratibu uliotambulishwa na UEFA wa kuwatumia waamuzi watano uwanjani sio mbaya lakini bado kuna umuhimu wa sheria ya kifaa hicho kutambulishwa kwa ajili ya kwenda sambamba na matukio ambayo mara kadhaa yamekua hayaonekani kwa uharaka.

No comments:

Post a Comment