Abeid Ayew Pele
George Manneh Oppong Ousman Weah
Baada ya kutwaa tuzo ya mchezaji bora barani Afrika kwa mara ya nne, mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Cameroon, pamoja na klabu ya Inter Milan Samuel Eto'o amewataka mashabiki wa soka barani humo kutomuona bora zaidi ya wengine.
Mshambuliaji huyo mwenye uimri wa miaka 29, ameyasema hayo siku moja baada ya kukabidhiwa tuzo hiyo mjini Cairo nchini Misri huku akiwabwaga wapinzani wake Asamoah Gyan kutoka nchini Ghana pamoja na Didier Drobga kutoka nchini Ivory Coast.
Samuel Eto'o amewataka mashabiki wa soka kutompa nafasi hiyo huku akieleza wazi kwamba kutwaa tuzo ya barani Afrika kwa mara ya nne haimaanishi yeye ni bora kuliko wachezaji wengine barani humo, bali ifahamike wapo na walikuwepo wenye uwezo mkubwa zaidi yake.
Amesema wapo wachezaji ambao yeye binafsi anawaheshimu na kuwatukuza kwa mchango mkubwa walioutoa katika vilabu na timu zao za taifa lakini hawakubahatika kufikia mafanikio aliyoyapata, hivyo amesisitiza kwamba wachezaji hao wanatakiwa kuheshimiwa pia na mashabiki wake.
Amesema mchezaji kama Abeid Ayew Pele ambae amefanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa bara la Afrika mara tatu, tayari ameshaifanyia makubwa nchi yake ya Ghana ambapo aliiwezeshwa kutwaa ubingwa wa barani Afrika katika miaka ya 90 sambamba na kufanya mengi mazuri katika klabu alizozitumikia nje ya bara la Afrika.
Samuel Eto'o pia akamzungumzia gwiji wa zamani toka nchini Liberia George Manneh Oppong Ousman Weah kwa kubainisha wazi kwamba anamuheshimu mchezaji huyo kwa uwezo wake aliouonyesha uwanjani na bado anauheshimu mchango wake alioutoa kwa kulitangaza bara la Afrika kupitia mchezo wa soka.
George Manneh Oppong Ousman Weah nae tayari ameshatwaa tuzo ya mchezaji bora wa bara la Afrika mara tatu.

No comments:
Post a Comment