KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, December 23, 2010

Leodger Chilla Tenga ATAJA KAMATI YA UCHAGUZI KENYA.


Shirikisho la soka duniani kote FIFA limewateua wajumbe wanane watakaosimamia uchaguzi mkuu wa shirikisho la soka nchini Kenya ambalo litafanya uchaguzi wake mwezi April mwaka 2011.

FIFA wameitangaza kamati hiyo kupitia kwa raisi wa shirikisho la soka nchini Tanzania Leodger Chilla Tenga ambae ameteuliwa kuwa msuluhishi wa masuala la soka nchini Kenya ambayo kwa muda mrefu yamekua katika mgogoro mkubwa.

Akiongoza mkutano wa waandihsi wa habari hii leo jijini Nairobi Leodger Chilla Tenga ambae pia ni raisi wa CECAFA amewataja wajumbe hao watakaounda kamati hiyo ya uchaguzi ambapo miongoni mwa wajumbe hao wapo wachezaji wa zamani wa kimataifa toka nchini Kenya Joe Masiga pamoja na Nahashon "Lule" Oluoch.

Tenga pia amemtaja mwanasheria Joe Okwach kuwa mwenyekiti wa kamati hiyo ambayo itakua na jukumu la kuwapata viongozi halali wa shirikisho la soka nchini humo katika uchaguzi mkuu wa mwezi April mwakani.

Amesema ana imani wajumbe hao aliwatangazwa hii leo kwa mapendekezo ya FIFA wataongoza uchaguzi kihalali na kuufanya kuwa na sifa za huru na haki hivyo wakenya wote wataridhika na viongozi watakaoingia madarakani.

Katika mkutano huo wa waandishi wa habari Leodger Chilla Tenga aliongozana na muwakilishi wa FIFA kutoka nchini Botswana Ashford Mamelodi.

Kama itafuatiliwa vyema nchi ya Kenya kwa kipindi cha miaka kadhaa imekua na mvutano wa kimadaraka katika mchezo wa soka kufuatia pande mbili kuvutana ambazo ni KFF pamoja na FKL huku kila upande ukitangaza kuwa na nguvu ya madaraka.

No comments:

Post a Comment