KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, December 24, 2010

KUONDOKA KWA SAMBA KUNANIUMIZA - STEVE KEAN.


Vugu vugu la usajili bado linaendelea kuwaumiza vichwa baadhi ya mameneja wa vilabu vya ligi kuu ya soka nchini Uingereza ambapo kila mmoja amekua akiweka hadharani mikakati ya kukitumia kipindi cha usajili wa dirisha dogo kitakachoanza mwishoni mwa juma lijalo.

Tayari baadhi ya mameneja wameshaeleza wazi kutaka kufanya usajili huku wengine wakibainisha kwamba hatofanya usajili kwa kuviamini vikosi vyao katika harakati za kusaka mafanikio msimu huu.

Meneja wa klabu ya Bluckburn Rovers Steve Kean ambae amepewa madaraka hayo mara baada ya kutimuliwa kazi kwa Sam Allardyce nae hii leo ameeleza mikakati yake ya usajili ambapo ameahidi kukiongezea nguvu kikosi chake kufuatia ahadi aliyopewa na uongozi mpya wa klabu hiyo.

Steve Kean amesema anajipanga kufanya hivyo kwa ajili ya kukamilisha mikakati aliyojiwekea klabuni hapo mara baada ya kukabidhiwa madaraka siku mbili zilizopita lakini akasisitiza kutokua tayari kumuuza mchezaji yoyote klabuni hapo.

Meneja huyo mwenye umri wa miaka 40, amesema lengo kubwa la kutokua tayari kumuuza mchezaji yoyote klabuni hapo katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo ni mikakati ya kuendelea kutengeza timu ya pamoja ambayo inaaminiwa itafikia mipango inayotarajiwa kwa siku za usoni sambamba na kuwatumia wachezaji chipukizi.

Hata hivyo Kean amezungumzia suala la beki wa kimataifa toka nchini Congo Brazzavile Christopher Samba kuomba nafasi ya kuondoka Ewood Park mwezi januari ambapo ameeleza kuwa suala hilo limemsikitisha na tayari ameshafanya mawasilino na wakala wa mchezaji huyo na amemthibitishia juu ya ombi hilo.

No comments:

Post a Comment