Meneja wa klabu ya Man city Roberto Mancini amekataa kata kata kuweka wazi mipango yake ya usajili kupitia dirisha dogo.
Roberto Mancini anaehusishwa na taarifa za kutaka kumsajili mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Serbia na klabu ya Wolfburg ya nchini ujerumani Edwin Dzeko amekataa kuzungumzia suala hilo huku akiwataka waandishi wa habari kumuuliza taarifa za michezo mitatu ya ligi inayoamuandama kuanzia mwishoni mwa juma hili.
Meneja huyo wa kimataifa toka nchini italia pia akakata kuzungumzia suala la Emmanual Adebayor na Wyane Bridge ambao wote kwa pamoja wanahusishwa na taarifa za kuuzwa mwezi januari mwaka 2011.
No comments:
Post a Comment