KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, December 24, 2010

UBINGWA UPO KWA MAN UTD, ARSENAL NA CGHELESEA TU !!


Meneja wa klabu ya Manchester Utd Sir Alex Ferguson ameingilia kati sakata la utabiri ambalo jana lilileta mzozo kati ya meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger dhidi ya mshambuliani wa kimataifa toka nchini Ureno Louis Nani ambae alitangaza kuwaondoa washika bunduki wa Ashburton Grove kwenye mbio za ubingwa msimu huu.

Sir Alex Ferguson ameingilia katika mzozo huo huku akionyesha kwenda tofauti na mshambuliaji wake Louis Nani ambapo amesema klabu ya Chelsea pamoja na Arsenal ndizo pekee zinakidhi vigezo vya kumuonyesha upinzani kwenye harakati za kusaka ubingwa msimu huu.

Amesema kimtazamo klabu hizo tatu zina uwezo wa kukidhi namna ya kutwaa ubingwa msimu huu kutokana na kuwa na wachezaji wenye uzoefu na mikimiki ya michezo iliyosalia hasa ikizingatiwa mbio za ubingwa huanza katika kipindi hiki cha sikuku za mwishoni mwa mwaka.

Ferguson pia akazungumzia kwa nini haipi nafasi ya kutosha klabu ya Manchester City pamoja na Tottenham ambapo ameeleza wazi kwamba vilabu hivyo havina mbinu mbadala za kukimbizana katika kipindi hiki na mara kadhaa vimekua vikionyesha mchezo kama homa za kupanda na kushuka yaani leo wanashinda kesho wanapoteza.

Man Utd ambao wapo kileleni mwishoni mwa juma hili watakua nyumbani wakiwakaribisha Sunderland kwenye uwanja wa Old Trafford huku wakionyesha matumaini makubwa ya kutanua wigo wa kipoint dhidi ya klabu nyingine.

Wakati huo huo chama cha soka nchini Uingereza hii leo kimetoa marekebisho ya ratiba ambayo yanaonyesha kuwa mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita ulioahirishwa kati ya Chelsea dhidi ya Man Utd sasa utachezwa tarehe moja mwezi wa tatu mwaka 2011.

Mchezo huo uliokua umepangwa kufanyika Desemba 19 mwaka huu uliahirishwa kufuatia hali ya hewa kutokua nzuri jijini London ambapo Chelsea walitarajiwa kuwa wageni huko Stamford Bridge.

Hata hivyo bado mchezo huo utachezwa uwanjani hapo kwa tarehe iliyopangwa.

Michezo mingine iliyoahirishwa mwishoni mwa juma lililopita nayo imepangwa tarehe nyingine ambapo mchezo hiyo ni kati ya;

Jumanne, 15 February 2011
Birmingham v Newcastle

Jumanne, 22 February 2011
Arsenal v Stoke
Blackpool v Tottenham
West Brom v Wolverhampton

No comments:

Post a Comment