KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, December 23, 2010

LABDA IWE MIUJIZA !!!


Meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amebadili msimamo na kueleza wazi huenda akafanya usajili wa mchezaji ama wachezaji katika kipindi cha usajili wa dirisha dogo, lakini amewataka mashabiki wa klabu hiyo kutotegemea miujiza.

Arsene Wenger ametoa msimamo huo, baada ya juma moja kupita ambapo alikaririwa na vyombo vya habari akisema msimu wa dirisha dogo huenda asifanye usajili wa mchezaji yoyote yule kufuatia kuwa na wachezaji wa kutosha ndani ya kikosi chake.

Mzee huyo wa kifaransa amesema pamoja na kurejesha matumaini ya kufanya usajili katika kipindi hicho, bado hatua hiyo itategemea kama kuna mchezaji atauzwa klabuni hapo katika kipindi cha dirisha dogo na kama itashinidikana basi ataendelea kuwatumia wachezaji waliopo kikosini.

Akitoa sababu ya kuwataka mashabiki kutotegemea miujiza Arsene Wenger amesema kwa sasa ni vigumu kumpata mchezaji atakaeweza kuisaidia klabu katika michuano ya barani Ulaya kutokana na wachezaji wengi wa barani humo kuwa tayari wameshazitumikia klabu zao katika michezo ya kimataifa.

Amesema endapo litajitokeza suala la kufanya usajili na akafanikiwa kumpata mchezaji ambae atakua bado hajachezea kwenye michuano ya kimataifa barani Ulaya, litakua suala la kimiujiza sana hivyo akaendelea kuwasisitizia mashabiki wa The Gunners kutojipa matumaini makubwa.

Katika hatua nyingine Arsene Wenger ameonyesha kufurahishwa na hatua ya kurejea kikosini kwa baadhi ya wachezaji wake ambao walikua majeruhi kwa kipindi cha majuma kadhaa lakini kwa bahati mbaya mzee huyo akaonyesha majonzi ya kuendelea kumkosa beki wa kimataifa toka nchini Ubelgiji Thomas Vermalen ambae anahitaji kipindi cha mwezi mmoja kwa ajili ya kujiweka fit kabla ya kurejea uwanjani kisawa sawa.

Amewataja wachezaji waliorejea kikosini ambao pia anatarajia kuwatumia katika mchezo wa mwanzoni mwa juma lijalo dhidi ya Chelsea kuwa ni Abou Diabi, Lucas Fabianski ambao walikosa michezo kadhaa iliopita huku Cesc Fabregas pamoja na Robin Van Parsie akiwataja kurejea kikamilifu.

Wakati huo huo Arsene Wenger ameonyesha kushangazwa na kauli iliyotolewa na mshambulaiji wa kimataifa toka nchini ureno na klabu ya Man Utd Louis Nani ya kuiondoa Arsenal katika mbio za ubingwa msimu huu na badala yake ametoa nafasi kwa klabu yake pamoja na Chelsea.

Wenger amesema ni kitendo cha aibu kwa mchezaji kama huyo kuzungumza kauli hiyo hadharani, hasa ukizingatia mlolongo wa michezo ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza kwa sasa umekua mgumu hali ambayo unaufanya msimamo wa ligi kuonyesha mbanano wa kipoint kati ya timu na timu.

No comments:

Post a Comment