Klabu bingwa barani Afrika TP Mazembe kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imekua klabu ya kwanza ya barani Afrika kutinga kwenye hatua ya fainali ya michuano ya klabu bingwa duniani baada ya kuwabanjua mabingwa wa soka wa barani Amerika ya kusini Internacional SC kutoka Brazil mabao mawili kwa sifuri.
Michuano hiyo inayofanyika mjini mjini Abu Dhabi huko Falme za kiarabu, ilishuhudia mabingwa hao wa bara la Afrika wakiweka rekodi ya kuwa klabu ya kwanza kutoka barani hapa kufika fainali kufuatia mabao yaliyopachikwa wavuni na washambuliaji Mulota Kabangu katika dakika ya 53 pamoja na Dioko Kaluyituka katika dakika ya 85.
Kabla ya kukutana na mabingwa wa soka barani Amerika ya kusini TP Mazembe walicheza mchezo wa kwanza dhidi ya ambingwa wa bara ya Amerika ya kati na kaskazini Club de Futbol Pachuca kutoka nchini Mexico.
Kwa hatua hiyo sasa TP Mazembe wanamsubiri mshindi wa mchezo wa hatua ya fainali unaopigwa hii leo kati ya mabingwa wa soka barani Ulaya Inter Milan ya Italia dhidi ya mabingwa wa soka barani Asia Seongnam IIhwa kutoka Korea Kusini.
Mchezo wa hatua ya fainali umepangwa kuchezwa jumamosi Disemba 18 mwaka huu.
No comments:
Post a Comment