KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, December 14, 2010

WENGER AMTABIRIA Wojciech Szczesny MAKUBWA ZAIDI.


Meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger amekubali matokeo ya mchezo wa jana ya kubamizwa bao moja kwa sifuri dhidi ya Man Utd waliokua nyumbani huko Old Trafford.

Wenger amesema kikosi chake kwa ujumla kilicheza vizuri lakini bahati ya ushindi haikuwa kwao na hilo lilijidhihirisha pindi walipokua wakisaka nafasi ya kusawazisha bao lililofungwa na Park ji Sung katika dakika ya 40.

Amesema kupoteza point tatu za mchezo wa jana ni somo kwao kuendelea kufanya juhudi ambazo zitawawezesha kufikia malengo waliyojiwekea msimu huu ya kutwaa ubingwa wa Uingereza ambao wamewaponyoka kwa miaka mitano iliyopita.

Arsene Wenger pia ameonyesha kumuamini kipa wake chaguo la tatu Wojciech Szczesny ambae alimpa nafasi ya kucheza mchezo wake wa kwanza wa ligi kuu na kuonyesha uwezo wa kumudu mikimiki ya wapinzani wao Man Utd.

Amesema kipa huyo mwenye umri wa miaka 20 ameonyesha uwezo wa kujiamini na amemtabiria makubwa katika siku za usoni kwenye mchezo wa soka uliomkuza.

Szczesny alipata nafasi ya kuitumia Arsenal kwa mara ya kwanza toka aliposajiliwa mwaka 2008,baada ya kipa chaguo la pili Lukasz Fabianski kuwa na maumivu ya mguu huku kipa chaguo la kwanza Manuel Almunia akiendelea kuuguza maumivu mkono.

Wakati huo huo mchezaji wa zamani wa klabu za Dundee United, Aston Villa, Wolverhampton Wanderers, Everton, Aston Villa, Notts County , West Bromwich Albion, Rangers pamoja na Cheltenham Town Andrew Mullen Gray ameonyesha kukikubali kiwango cha uchezaji wa klabu ya Arsenal walichokionyesha wakati wa kipindi cha pili cha mchezo huo wa jana, lakini akasema kikwazo cha uchezaji huo mzuri kilikua ni ulinzi mkali uliowekwa na Man Utd.

Andrew Mullen Gray pia ameonyesha kuchukizwa na maamuzi ya utoaji wa panati ambayo amesema hayakua sahihi kimtazamo licha ya Gael Clich kuushika mpira katika eneo la hatari, lakini mshika kibendera hakua na uhakika wa kutosha hatua ambayo ilipelekea kuchelewa kumshawishi muamuzi Howard Webb kupuliza filimbi na kuamuru mkwaju wa penati upigwe kuelekea katika lango la Arsenal.

No comments:

Post a Comment