Serikali ya nchini Zambia inatarajia kutuma ujumbe wa watu sita kwenda mjini Zurich nchini Uswiz yalipo makao makuu ya shirikisho la soka duniani FIFA kwa lengo la kujadili masula mbali mbali yanayopelekea mvurugano uliopo ndani ya chama cha soka nchini humo.
Ujumbe huo wa watu sita unatarajia kuelekea mjini Zurich baada ya raisi wa nchini Zambia Rupiah Banda kuomba nafasi kwa raisi wa FIFA Sepp Blatter kuzungumza namna ya kutatua matatizo yanayoendelea nchini kwake kupitia mchezo wa soka.
Maombi ya Rupiah Banda kwa Sepp Blatter yalilenga zaidi kusaka ushauri wa nini kifanyike ili kumaliza matatizo yanayoendelea kati ya raisi wa chama cha soka nchini Zambia Kalusha Bwalya dhidi ya wadau wa soka nchini humo wanaoongozwa na mfanya biashara maarufu Andrew Kamanga ambao hawamtaki kwa namna yoyote ile aendelee na utawala wake wa kuiongoza FAZ.
Ujumbe huo wa watu sita tayari umeshateuliwa na raisi Rupiah Banda ambapo ametaka pande hizo mbili kutoa wawakilishi wawili, wawili na upande wa serikali utatoa wawakilishi wawili ambao anaamini watakapokuwa mujini Zurich watapata namna ya kumaliza matatizo ambayo yeye binafsi amekiri yanamkera kupita kiasi.
Ujumbe huo wa watu sita kutoka nchini Zambia umepangiwa kukutana na uongozi wa FIFA Desemba 21 mwaka huu.
Kalusha Bwalya, ambae alikua mchezaji bora wa barani Afrika mwaka 1998 amekua na mvutano wa hali ya juu na wadau wa soka nchini humo hatua ambayo imepelekea wajumbe wa kamati ya utendaji wa chama cha soka kujiuzulu nafasi zao kwa lengo la kumshinikiza aachie madaraka.
Sababu kubwa inayotajwa kwa mwanandinga huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Zambia ni kujichukulia maamuzi yeye binafsi mbali na mikakati ya chama inavyopagiza hali ambayo imekuwa ikidaiwa kulilipeleka pabaya soka la nchini Zambia.

No comments:
Post a Comment