Meneja wa klabu ya Man City Roberto Mancini ameulaumu wazi wazi utaratibu wa upangaji wa ratiba ya ligi kuu ya soka nchini Uingereza ambayo katika msimu huu wa sikuku imenaonekana kuvibana vilabu kwa kucheza michezo mingi kwa siku chache zilizosalia kabla ya mwaka mpya.
Mancini ameulaumu utaratibu huo muda mchache tu mara baada ya kikosi chake kufanikisha suala la ushindi mbele ya Aston Villa hapo jana ambapo amesema kwa asilimia kubwa ya wachezaji wanaocheza ligi hiyo wamekua wakichoka hivyo inamlazimu yeye pamoja na mameneja wengine kufanya mabadiliko yasiyo ya lazima.
Amesema kikosi chake kilicheza mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Newcastle Utd na kisha baada ya siku moja kikacheza mchezo mwingine dhidi ya Aston Villa hali ambayo ameizungumza ni kama ukatili unaofanywa kwa wachezaji ambao amedai wanahitaji kupumzika.
Akijitolea mfano yeye binafsi kupitia mchezo wa jana meneja huyo wa kimataifa toka nchini Italia amesema ilimlazimu kufanya mabadiliko ya wachezaji wa tano katika kikosi chake kwa lengo la kuwapumzisha wachezaji wengine ambao mwishoni mwa juma hili wanakabiliwa mchezo dhidi ya Blackpool.
No comments:
Post a Comment