Raisi wa klabu bingwa barani Ulaya pamoja na ulimwenguni kote Inter Milan Massimo Moratti amepatwa na kigugumizi pale alipotakiwa kuzungumzia mustakabali wa meneja wa klabu hiyo Rafael Benitez.
Massimo Moratti amefikwa na hali hiyo alipotakiwa na waandishi wa habari kuzungumza lolote juu ya Rafael Benitez, baada ya klabu yake kufanikiwa kutwaa ubingwa wa dunia mwishoni mwa juma lililopita kufuatia kisago cha mabao matatu walichokitoa kwa mabingwa wa barani Afrika TP Mazembe.
Morrati amesema kwa sasa haweezi kuzungumza lolote juu ya meneja huyo, lakini akaahidi ipo siku atazungumza nini ambacho anafikiria kuhusiana na Rafael Benitez ambae siku za hivi karibuni kibarua chake kilikua katika hali ngumu kufuatia matokeo mabovu yaliyokua yakimuandama.
Mbali na Massi Moratti kushindwa kuzungumzia mustakabali wa meneja wake, hatua za kutwaa ubingwa wa dunia mwishoni mwa juma lililopita zimeonyesha kumpa jeuri Rafael Benitez ambapo mara baada ya mchezo wa fainali alitamba mbele ya vyombo vya habari ambapo alisema kikosi chake ni bora na kimefanikiwa kufikia malengo hayo kutokana na kuwa na meneja mwenye ubora.
Amesema mpaka wanafikia hatua ya kutwaa ubingwa wa dunia, hajawahi kutumia fedha yoyote ya klabu hivyo hatua hiyo inajidhihirisha ni vipi alivyo makini katika harakati za kuwatumia wachezaji waliopo ambao wamewezesha ushindi uliopatikana.
No comments:
Post a Comment