Baada ya kushindwa kutwaa ubingwa wa dunia upande wa klabu, uongozi wa ngazi za juu wa klabu ya TP Mazembe umeahidi kufanya makubwa zaidi kwenye michuano hiyo ya dunia ya mwaka 2011.
Kauli hiyo ya kutia moyo kwa mashabiki wa klabu hiyo ambayo ni bingwa mara mbili mfululizo wa bara la Afrika imetolewa na raisi wa TP Mazembe Moise Katumbi ambapo ameahidi kufanya kila juhudi kuhakikisha wanapata nafasi nyingine ya kucheza michuano hiyo ya dunia.
Kauli hiyo ya kutia moyo ya Moise Katumbi ameiutoa saa kadhaa kabla ya kikosi cha TP Mazembe hakijaondoka mjini Abu Dhabi yalipokua yakifanyika mashindano hayo ambayo yameshuhudia mabingwa wa barani Ulaya Inter Milan wakitawazwa kuwa mabingwa wa dunia kwa ushindi wa mabao matatu kwa sifuri.
Amesema kocha wao amebaini makosa mengi yaliyopelekea kushindwa kutimiza malengo waliyokua wamejiweke kwenye michuano hiyo lakini akaahidi huu ndio muda wa kuanza kujipanga na kutiza mikakati ya kurejea tena kwenye michuano hiyo mikubwa ambayo imewakutanisha na klabu nguli duniani.
Kurejea kwa TP Mazembe katika michuano hiyo, itawalazimu kutetea ubingwa wa barani Afrika kwa mara ya tatu mfululizo, hali mbayo itakua na upinzani mkubwa kwao kutokana na vilabu vingine barani humo kujipanga kisawa sawa.
No comments:
Post a Comment