KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, December 15, 2010

MENGI YAMEKIUKWA KWENYE MKATABA WAKE !!


Wakala wa soka toka nchini Israel Kia Joorabchian amemtaka mtendaji mkuu wa klabu ya Man city Garry Cook kutafuta namna ya kumaliza mgogoro uliojitokeza kati ya uongozi wa klabu hiyo dhidi ya mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Argentina na si kuamua masuala hayo kibabe.

Kia Joorabchian ambae alikua akimmiliki mshambuliaji huyo miaka kadhaa iliyopita ametoa ushauri huo baada ya kuonyesha kuchukizwa na utaratibu unaoendelea huko City Of manchester ambao unaonyesha kutomtendea haki Tevez ambae amekiri hafurahishwi na maisha ya klabu yake ya sasa.

Kia amesema jukumu kubwa la Garry Cook kwa sasa ni kusaka mbinu tofauti za kubadili mfumo wa uongozi wake na kutambua umuhimu wa wachezaji ambao ni bora zaidi yake klabuni hapo na endapo atashindwa kufanya hivyo, kuna uwezekano mkubwa wa malengo ya klabu hiyo kutokufikiwa.

Amesema Tevez ilimlazimu kueleza wazi kwamba yu tayari kuondoka City Of Manchester kufuatia kuchukizwa na baadhi ya watendaji wa juu wa klabu ya Man City, hatua ambayo ameifafanua kwa kueleza kwamba mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26 hajatimiziwa mambo yake mengi aliyoahidiwa.

Akibainisha wazi baadhi ya mambo hayo Kia Joorabchian ametanabai kuwa Tevez alitakia kuboreshiewa mkataba wake kwa makubaliano aliyokubaliana na uongozi wake wakati akijiunga na Man City kipindi cha usajili msimu uliopita sambamba na kuchukizwa na maamuzi ya meneja Roberto Mancini ambae anadai kutomtendea haki ya kumpa nafasi ya kucheza kama ilivyokua siku za nyuma wakati wa utawala wa Mark Hughues.

Sababu kubwa ya Kia Joorabchian kumtaka Garry Cook asake mbinu mbadala za kumaliza tatizo la Teves ni kutokana na kauli aliyoitoa ambayo ilikwenda kinyume na ombi lilowasilishwa ofisini kwake na mshambuliaji huyo ambalo lililenga kutaka ruhusa ya kuondoka mwezi januari.

Wakati huo huo, mchambuzi wa masuala ya soka nchini Uingereza pamoja na mwanandinga wa zamani wa nchini humo Paul Mccarthy nae ameonyesha kuunga mkoano mpango wa kutafutwa kwa muafaka ambao utamuwezesha Tevez kusaka maisha ya soka kwingine mwishoni mwa msimu huu.

Pia mchambuzi huyo akatoa ushauri kwa uongozi wa Man City ambapo ameutaka kumsajili mshambuliaji toka nchini Bosnia pamoja na klabu ya Wolfburg ya nchini Ujerumani Edwin Dzeko endapo mshambuliaji huyo wa Argentina ataamua kuondoka.

No comments:

Post a Comment