Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Sierra Leone Mohammed Kallon anajipanga kuachana na klabu yake ya sasa nchini China Shaanxi Chanba.
Kallon ametangaza hadharani dhamira hiyo huku mkataba wake ukitarajia kumalizika Desemba 31 mwaka huu na ameeleza wazi kwamba hatokua tayari kusiani mktaba mwingine na uongozi wa klabu hiyo ambayo ameitumikia kwa kipindi cha miezi kumi iliyopita.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 31, amesema dhamira yake kubwa ya kutosaini mkataba mwingine na uongozi wa klabu hiyo ni kutaka kuwa karibu na familia yake ambayo inaishi nchini Marekani ambapo inahisiwa huenda akacheza katika moja ya klabu za nchini humo.
Hata hivyo ameelza kwamba uongozi wa klabu yake ya sasa umemtaka kuongeza mkataba mwingine lakini suala hilo limeshindikana na ameshaueleza wazi dhamira yake ni kutaka kuwa karibu na familia yake ambayo aliihamisha nchini China kwa lengo kutaka kumpa nafasi mwanae wa kike kusoma shule zinazofundisha kiingereza ambazo amedai mjini Xian nchini China anapoishi kwa sasa shule hizo hakuna.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa klabu bingwa duniani Inter Milan ya nchini Italia pamoja na AS Monaco ya nchini Ufaransa hakusita kubainisha mustakabali wake mara baada ya kuondoka nchini China, ambapo amesema huenda akacheza soka nchini Marekani ama katika nchi yoyote ya Barani ulaya ama Asia kufuatia klabu kadhaa za nchi hizo kuonyesha nia ya kutaka kumsajili.
Licha ya kukiri kuwepo kwa uhakika wa kujiunga na moja ya klabu za nchi za maraba aliyoyataja Mohammed Kallon amesema mara baada ya mkataba wake kumalizika Desembe 31, anataka kupumzika kwa muda wa siku kadhaa na maamuzi rasmi ni wapi atakapoelekea atayatoa mwezi Januari mwaka 2011.
No comments:
Post a Comment