Aliekua meneja wa klabu ya Blackburn Rovers Sam Allardyce amesema alishtushwa na maamuzi ya kutimuliwa kazi klabuni hapo na wamiliki wapya wa klabu hiyo jana jioni.
Sam Allardyce amesema kabla ya maamuzi ya kutimuliwa klabuni hapo hayajachukuliwa alifanya kikao na mabosi wake ambao walimueleza wazi kwamba hafurahishwi na mwenendo wa kikosi chao hivyo wangetamani kuona mwenendo mzuri siku za hivi karibuni unaanza kuonekana.
Amesema yeye binafsi alikua hana wazo lolote kama angeweza kutimuliwa kazi lakini mara baada ya kikao hicho kufanyika alisikitishwa na maamuzi yaliyochukuliwa na mabosi wake ambao walimtakia kila la kheri katika maisha yake baada ya kuondoka huko Ewwod Park.
Amesema aliipenda sana klabu hiyo na alitambua huenda wamiliki hao wangemuwezesha kutimiza malengo yake ya kufanya vyema msimu huu kwa kufanya usajili wa wachezaji mwezi januari lakini ndoto zake zimekatishwa na sasa anafikiria kuanza maisha mengine ya umeneja ndani ya klabu nyingine itakayomuhitaji.
Katika hatua nyingine Sam Allardyce amewashukuru wote waliokua nae bega kwa bega katika mikakati aliyojiwekea klabuni hapo, pia amewatakia kheri wachezaji wa klabu hiyo pamoja na uongozi wa Rovers.
Blackburn Rovers kwa sasa inamilikiwa na wanandugu wawili ambao ni Balaji Rao pamoja na Venkatesh Rao kutoka nchini India.
Wakati huo huo wamiliki hao ametoa msimamo wao uliopelekea kuchukua maamuzi ya kumtimua kazi Sam Allardyce ambapo wamesema meneja huyo wa kiingereza alikua hana mtazamo wa kukiwezesha kikosi chao kutimiza malengo waliyojiwekea msimu huu.
Wamiliko hao wamesema malengo yao waliyojiwekea ni kuhakikisha kikosi cha Rovers kimaliza katika nafasi ya nne ama ya tana kwenye msimamo wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza ili kiweze kupata nafasi ya kushiriki michuano ya vilabu ya barani ulaya.
No comments:
Post a Comment