KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, December 16, 2010

Roberto Mancini AAHIDI KUZUNGUMZA NA TEVEZ.


Sakata la mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Argentina Carlos Tevez la kutaka kuondoka huko City Of Manchester limechukua sura mpya, ambapo kwa kipindi hiki meneja wa klabu hiyo Roberto Mancini imemlazimu kuingilia kati na kuahidi kesho atafanya mazungumzo na mshambuliaji huyo.

Ahadi hiyo ya Mancini ameitoa mbele ya waandishi wa habari alipozungumzia mchezo wa hii leo ambapo Man city watakua ugenini wakicheza na Juventus kwenye michuano ya ligi ya barani Ulaya.

Amesema imani yake kubwa inamtuma mazungumzo kati yake ya mshambuliaji huyo yatafikia muafaka na Tevez atarudisha moyo wake wa kuendelea kuitumia Man city ambayo bado inamuhitaji kwa asilimia 100.

Hata hivyo meneja huyo wa kimataifa toka nchini Italia amebainisha wazi kwamba litakua jambo la kipuuzi endapo watashindwa kuafikiana na mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 26.

Amesema kwa sasa wapo katika nafasi nzuri kwenye msimamo wa ligi na katika michuano mingine wanaendelea vyema, hivyo bado wanahitaji wachezaji kama Tevez na wengine kwa ajili ya kufikia malengo waliyojiwekea msimu huu.

Kama itakumbukwa vyema mwanzoni mwa juma hili Carlos Tevez aliibua sakata la kutaka kuondoka huko City Of Manchester huku akidai kuna baadhi ya mambo na baadhi ya viongozi klabuni hapo wamekuwa wakikwamisha masuala mbali mbali dhidi yake.

Hata hivyo licha ya kuibua sakata hilo mshambuliaji huyo alidiriki kuuandikia barua uongozi wa Man City kwa kuuomba ruhusa ya kuondoka katika kipindi cha dirisha dogo la usajili mwezi januari mwaka 2011, lakini ombi hilo limegongwa mwamba baada ya kukataliwa.

No comments:

Post a Comment