KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, December 25, 2010

SINA BUDI INANILAZIMU KUWAUZA TU !!


Meneja wa klabu ya Tottenham Hortspurs Harry Redknapp amesema hana budi kuwatoa wachezaji wake wawili katika kipindi cha dirisha dogo la usajili ambacho kitaanza mwishoni mwa juma lijalo.

Harry Redknapp ameweka wazi mpango huo huku akiwataja wachezaji hao kuwa ni beki wa kiingereza Jonathan Woodgate pamoja na mshambuliaji wa kimataifa toka Jamuhuri ya Ireland Robie Kean.

Amesema Jonathan Woodgate ambae kwa kipindi kirefu amekua akisumbuliwa na maumivu ya nyonga anatarajia kumtoa kwa mkopo baada ya kupona jeraha lake na amekua na hamu ya kucheza soka kama ilivyokua siku za nyuma, hivyo ameona ni bora amuuze kwa mkopo lakini hakueleza anampeleka kwenye klabu gani.

Kwa upande wa Robbie Kean, Harry Redknapp amesema mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 30 yupo kwenye mipango ya kuuzwa moja kwa moja kutokana na kukosa nafasi katika kikosi chake cha kwanza ambacho kwa sasa kina wachezaji kama Peter Crouch, Giovani dos Santos, Jermain Defoe pamoja na Roman Pavlyuchenko.

No comments:

Post a Comment