Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Uingereza na klabu ya Arsenal Theo James Walcott amesema endapo wachezaji wa soka wataendelea na mfumo wa kuwatuhumu waamuzi kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter kuna hatari kubwa kwao kujichimbia kaburi lao wenyewe.
Theo James Walcott ameyasema hayo alipozungumza na waandishi wa habari kwenye kambi ya timu ya taifa ya Uingereza ambapo amebainisha wazi kwamba wachezaji wengi kwa siku za hivi karibuni wamekua na mfumo mbovu wa kutumia mtandao huo wa kijamii kuelezea hasira zao mara wanapotoka uwanjani hali ambayo amedai si nzuri hata kidogo.
Amesema endapo wataendelea na mchezo huo kuna kila sababu ya wengi wao kufungiwa na vyama vya soka vya nchi husika hivyo ni jukumu la kila mmoja kuacha kabisa mchezo huo wa kutumia ovyo mtandao huo wa kijamii endapo wanahitaji kucheza soka kwa raha mustarehe.
Alipoulizwa kama yeye hupenda kutumia mtandao huo, Walcott alijibu hajawahi na wala hatowahi kuutumia mtandao huo ambao pia amedai hajua hata unafanana na rangi gani hapa ulimwenguni.
Walacott ameyaeleza hayo ikiwa ni siku tatu kupita baada ya mchezaji mwenzake wa klabu ya Arsenal Jack Andrew Garry Wilshere kuhusishwa na taarifa za kuandika ujumbe kupitia mtandao wa Twitter ambapo alieleza wazi namna alivyokerwa na muamuzi Phil Dowd aliechezesha pambano kati ya Newcastle Utd dhidi ya Arsenal lililomalizika kwa matokeo ya sare ya mabao manne kwa manne.
Hata hivyo tayari winga wa zamani wa klabu ya Liverpool Ryan Guno Babel ameshafikwa na mkasa wa kutozwa faini ya paund elfu 10, baada ya kukutwa na hatia ya kumdhalilisha muamuzi Webb Howard ambae alimuweka kwenye mtandao huo kwa picha za kutenegeneza huku akiwa mevalia jezi za klabu ya Man Utd kwa kaushiria ni mnazi mkubwa wa klabu hiyo ya Old Trafford.
No comments:
Post a Comment