KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, February 9, 2011

Gary Speed ACHUKUA TATU KUTOKA KWA Giovanni Trapattoni.

Republic of Ireland 3-0 Wales

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Wales Garry Speed usiku wa kuamkia hii leo alishikwa na kigugumizi, baada ya kikosi chake kukubali kisago cha mabao matatu kwa sifuri kutoka kwa Jamuhuri ya Ireland.

Garry Speed ambae jana alikua kazini kwa mara ya kwanza toka alipopewa jukumu la kukiongoza kikosi cha timu ya taifa ya Wales amesema licha ya kufungwa mabao hayo kikosi chake hakikucheza vibaya na hilo limejidhihirisha katika dakika 45 za kipindi cha kwanza kabla ya kukubali kirahisi kufungwa mabao yote matatu ndani ya kipindi cha pili.

Amesema amejifunza mengi na ana imani kikosi chake kitaendelea kubadilika siku hadi siku, hivyo anaamini watafanya vyema katika michezo ya kuwania kucheza fainali za mataifa ya ulaya za mwaka 2012.


Matokeo ya michezo mingine ya kimataifa ya kirafiki iliyochezwa usiku huu ni pamoja na:

Cyprus 0 - 2 Sweden
Ivory Coast 1 - 0 Mali
Romania 4 - 6 Ukraine
Ghana 4 - 1 Togo
Ireland 3 - 0 Wales
Peru 1 - 0 Panama

Egypt 0-0 USA

Michezo itakayochezwa leo tarehe 09-02-2010

Scotland v Northern Ireland

Greece v Canada

Iran v Russia

Croatia v Czech Republic

Israel v Serbia

Turkey v South Korea

Denmark v England

Belgium v Finland

Malta v Switzerland

Netherlands v Austria

Poland v Norway

Germany v Italy

Argentina v Portugal

France v Brazil

Spain v Colombia

No comments:

Post a Comment