Kocha mkuu wa timu ya taifa Wales Gary Andrew Speed amesema yu tayari kwa jaribio la kwanza la kukishuhudia kikosi cha nchi hiyo kikishuka dimbani kikiwa chini yake kwa kucheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Jamuhuri ya Ireland.
Gary Andrew Speed amesema anakwenda katika mchezo wa hii leo huku akibaini kuwa ni changamoto kubwa sana kwake pamoja na kikosi chake ambacho anaamini kitafanya vyema mbele ya kikosi cha Giovanni Trapattoni.
Amesema kila mmoja wao huko nchini Wales anatambua mchezo huo ni wa kujipima nguvu kabla ya kuendelea na mchakato wa kusaka nafasi ya kucheza fainali za mataifa ya bara la Ulaya kwa mwaka 2012, lakini kwake anauchukulia kama sehemu ya mashindano ambayo yatamuwezesha kila mmoja ndani ya kikosi kujua nini kinachohitajika katika kipindi hiki.
Mchezo wa kwanza wa mashindano kwa Gary Andrew Speed utachezwa March 26 mjini Cardiff nchini Wales dhidi ya timu ya taifa ya Uingereza iliyo chini ya kocha wa kimataifa toka nchini Italia Fabio Capello.
Gary Andrew Speed mwenye umri wa miaka 41 alikichukua kikosi cha timu ya taifa ya Wales mwishoni mwa mwaka 2010, huku akiwa tayari ameshakiongoza kikosi cha klabu ya Sheffield United kama meneja kwa muda wa miezi minne.
Michezo mingine wa kimataifa ya kirafikia mbayo itachezwa hii leo ni pamoja na;
Mozambique vs Botswana
Ghana vs Togo
Ivory Coast vs Mali
Cyprus v Sweden
Romania v Ukraine
Peru v Panama
No comments:
Post a Comment