KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Saturday, February 5, 2011

ADHABU ZIPO PALE PALE !!!!!!.


Kamati ya rufaa ya shirikisho la soka ulimwenguni kote imeziweka kapuni rufaa zilizowasilishwa huko mjini Zurich na wajumbe wa shirikisho hilo waliofunguwa kujishughulisha na masuala ya soka baada ya kukutwa na hatia ya kuomba rushwa mwishoni mwa mwaka jana.

Kamati ya rufaa ya FIFA imefikia maamuzi hayo baada ya kufuatia taarifa ya kamati ya nidhamu iliyofikia maamuzi ya kuwafungia wajumbe hao sambamba na kusikiliza upande wa watuhumiwa na kubaini kulikua kuna haki ya wahusika hao kufungiwa.

Majibu yalitolewa na kamati ya rufaa yameendelea klushikia msimamo ule ule ambao unamfanya Amos Adamu kutoka nchini Nigeria, kuendelea na kifungo chake cha miaka miwili, na hatoawani tena nafasi ya ya ujumbe wa FIFA katika uchaguzi wa CAF unaotarajiwa kufanyikwa mwishoni mwa mwezi huu huko nchini Khartoum nchini Sudan.

Reynald Temarii kutoka nchini Haiti anaendelea na kifungo chake cha kutoutumikia mchezo wa soka kwa kipindi cha mwaka mmoja.

Mbali na wajumbe hao wawili pia kamati ya rufaa ya FIFA imetangaza kuwapunguzia adhabu weajumeb wengine wa FIFA waliokata rufaa ya kupinga adhabu ambapo wajumbe hao ni Amadou Diakite kutoka nchini Mali, Slim Aloulou kutoka nchini Tunisia pamoja na Ahongalu Fusimalohi kutoka nchini Tonga.

Slim Aloulou: yeye amepunguzi wa adhabu kutoka miaka miwili hadi mwaka mmoja na ametakiwa kulipa faiani ya Franga za Ufaransa 5000 badala ya 10,000.

Amadou Diakité: amepunguziwa adhabu ya kutoka miaka mitatu hadi miaka miwili na ametakiwa kulipa fainai ya Franga za Ufaransa 7,500 badala ya 10,000.

Ahongalu Fusimalohi: amepunguziwa adhabu ya kutoka miaka mitatu hadi miaka miwili na ametakiwa kulipa fainai ya Franga za Ufaransa 7,500 badala ya 10,000.

No comments:

Post a Comment