Wakati sakata la usajili likiendelea kuwa gumzo huku msimu wake ukifikia tamati, huko Stamford Bridge yalipo makao makuu ya klabu ya Chelsea taarifa zimeelza kwamba uongozi wa klabu hiyo upo katika mchakato mkali wa kutaka kurejesha fedha zilizotumika kwenye usajili wa Fernando José Torres Sanz pamoja na David Luiz Moreira Marinho ambazo ni Paund Million 75.
Uchunguzi uliofanywa na moja ya chombo cha habari nchini Uingereza umebaini kuwa mchakato wa kusaka fedha hizo ili ziweze kurejea mikononi mwa Tycoon wa kirusi Roman Abramovich ambae pia ni mmiliki wa klabu hiyo ya jijini London ni kuuzwa kwa baadhi ya wachezaji klabuni hapo mwishoni mwa msimu huu.
Wachezaji wanaotajwa huenda wakauzwa mwishoni mwa msimu huu ni mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Ivory Coast Didier Yves Drogba Tébily, kiungo wa kimataifa toka nchini Nigeria John Michael Nchekwube Obinna *John Obi Mikel*, beki wa kimataifa toka nchini Ureno José Bosingwa da Silva, kiungo wa kimataifa toka nchini Ufaransa Florent Johan Malouda pamoja na kiungo wa kimataifa toka nchini Urusi Yuri Zhirkov.
Majibu ya uchunguzi huo yameendelea kueleza kwamba wachezaji hao wanatajiwa kuuzwa klabuni hapo kufutia viwango vyao kuwa tofauti na walivyosajiliwa siku za nyuma.
Wakati huo huo majibu ya uchunguzi huo yameendelea kuonyesha kwamba klabu ya Chelsea huenda ikaingia kwenye mzozo mkubwa na shirikisho la soka barani ulaya UEFA, kufuatia kutumia kiasi kikubwa cha fedha ambacho kinakwenda kinyume na hasara waliyoitangaza ya paund million 70.9.
No comments:
Post a Comment