KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, February 3, 2011

Alberto Suarez Diaz AMSHANGAZA DALGLISH.


Meneja wa klabu ya Liverpool King Kenny Dalglish amekiri kushangazwa na hatua ya mshambuliaji wake mpya Luis Alberto Suarez Diaz kucheza kwa ushirikiano mkubwa na wachezaji wengine klabuni hapo katika mchezo wa usiku wa kuamkia hii leo dhidi ya Stoke City.

Dalglish amebainisha wazi kwamba mshambuliaji huyo toka amewasili klabuni hapo hakuwahi kufanya mazoezi na wenzake na kama inakumbukwa vyema Luis Suarez ametoka nchini Uholanzi huku akiwa katika kifungo cha kutokucheza michezo sita ya ligi kufuatia kosa la kumng’ata begani mchezaji wa klabu ya Fayenhood Ottman Bakar.

Amesema alifanya kusudi kumuweka benchi mshambulaiji huyo na kujaribu kumchezesha katika kipindi cha pili na matokeo yake alishangazwa na hatua ya uchezaji wake mzuri ambayo ilimpelekea kupachika bao lake la kwanza ambalo lilikua ni bao la pili kwenye mchezo huo.

No comments:

Post a Comment