Mashabiki wa klabu ya Newcastle Utd wametakiwa kufungua ukursa mpya baada ya kuondoka kwa mshambuliaji wao wa kimataifa toka nchini Uingereza Andy Carroll aliejiunga na klabu ya Liverpool usiku wa kuamkia Februari Mosi.
Rai hiyo kwa mashabiki hao imetolewana meneja wa Newcastle utd Allan Pardew ambapo amesema kuondoka kwa mshambulaiji huyo hakuna namna ya kuendelea kuzungumzwa klabuni hapo zaidi ya kuendelezwa kwa mshikamano ambao utaleta mafanikio zaidi hadi mwishoni mwa msimu huu.
Amesema mshambulaiji huyo alikuzwa na klabu ay Newcastle Utd na kuondoka kwake ni sehemu yamaisha yake ya soka, hivyo hakuna haja ya kuendelea kuhoji kwa nini ameondoka tena kwa ada ya uhamisho wa paund million 35 ambayo imekua ikizumngumzwa kwa mazuri na mabaya na mashabiki wa soka nchini Uingereza.
Mbali na rai hiyo kutolewa kwa mashabiki pia Allan Pardew aliielekezea kwa wachezaji wa kikosi chake ambapo amewataka kuendelea kuonyesha bidii zaidi.
No comments:
Post a Comment