Raisi wa shirikisho la soka barani Afrika CAF, Issa Hayatou amesema kamwe hatothubutu kuwania nafasi ya uraisi wa shirikisho la soka ulimwenguni kote FIFA, dhidi ya raisi wa sasa wa shirikisho hilo Joseph Sepp Blatter.
Issa Hayatou ametoa msimamo huo mjini Kharatopum nchini Sudan alipozungumza na vyombo vya habari ambapo amesema ni vigumu kuwa mpinzani wa Blatter katika kuwani kiti cha uraisi wa FIFA na yeye binafsi alilitambua hilo mwaka 2002 alipoweka dhamira ya kutaka kuwa kiongozi wa juu wa soka duniani.
Amesema mwaka huo dhamira yake ilikua ni kutaka kuwa raisi wa FIFA, na ndio maana alijitosa kuwania nafasi hiyo lakini alikumbana na upinzani mzito kutoka kwa Blatter ambae anakubalika kwa asilimia kubwa ulimwenguni kote kwa misingi mizuri ya soka aliyoijenga.
Issa Hayatou mwenye umri wa miaka 64, ameweka dhamira hiyo ya kutogombea uraisi, huku uchaguzi wa kuwania uraisi wa FIFA ukitarajiwa kufanyika mwezi June mwaka huu na tayari raisi wa shirikisho la soka barani Asia Mohamed Bin Hammam ametangaza kuwania nafasi hiyo sambamba na Blatter.
No comments:
Post a Comment