KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, February 2, 2011

ANCELOTTI KUMTUMIA TORRES JUMAPILI.


Meneja wa klabu ya Chelsea Carlo Michelangelo Ancelotti amethibitisha taarifa za kutarajia kumtumia mshambuliaji mpya wa klabu hiyo Fernando José Torres Sanz mwishoni mwa juma hili pale jeshi la Taykun wa kirusi Roman Abramovic litakapokua nyumbani Stamford Bridge kucheza na Liverpool.

Ancelotti ametoa uthibitisho huo usiku wa kuamkia hii leo mara baada ya mchezo wa ligi uliochezwa huko Stadium of Lights ambapo amedai kwamba Fernando José Torres Sanz yu tayari kukitumikia kikosi chake kufuatia hamu aliyo nayo ya kutaka kucheza na klabu yake ya zamani ya Liverpool.

Amesema mshambuliaji huyo aliewagharimu kiasi cha paund million 50 kilichotumika kwenye ada ya uhamisho wake, atawafaa kwa kipindi hiki cha ushindani kufuatia umahiri wake anapokua uwanjani na hiyo ndio sifa kubwa iliyosababisha amvute jijini London.

Mbali na Fernando José Torres Sanz pia Anceloti amethibitisha kutarajia kumtumia beki mpya wa kimataifa toka nchini Brazil David Luiz Moreira Marinho aliesajiliwa huko magharibi mwa jiji al London kwa kiasi cha paund million 21.4 akitokea kwenye klabu ya Benfica ya nchini Ureno.

Wakati huo huo mzee huyo wa kitaliano mwenye umri wa miaka 51 ameonyesha hatua ya kufurahishwa na mabadiliko makubwa yaliajitokeza ndani ya kikosi chake ambacho jana kilijikuta kikipachikwa bao katika dakika ya nne na wapinzani wao Sunderland.

Amesema baada ya bao hilo wachezaji wake walionyesha kutulia na kufanya jitihada za kusawazisha na mwisho wa mchezo walifanikiwa kuondoka na ushindi wa mabao manne kwa mawilia mbao unathibitishia wapo tayari kutetea ubingwa wao kwa mara nyingine tena baada ya kusua sua mwishoni mwa mwaka uliopita.

Ushindi huo wa mabao manne kwa moja unaendelea kuwaweka Chelsea katika nafasi ya nne kwa kufikisha point 44 nyuma ya Man city wenye point 45 huku ikiwa ni tofauti ya point 10 dhidi ya vinara wa ligi hiyo Man Utd.

No comments:

Post a Comment