KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, February 2, 2011

SPURS YAKOSA WACHEZAJI MUHIMU.


Baada ya kumkosa Chalie Adam ndani ya dakika mbili baada ya dirisha dogo la usajili kufujafungwa usiku wa kuamkia jana huko barani Ulaya, meneja wa klabu ya Tottenham Hotspurs Henry James "Harry" Redknapp ameendelea kueleza masikitiko yake ya kuwakosa wachezaji wengine ambao alitarajiwa kuwapata ndani ya usiku huo.

Henry James "Harry" Redknapp amesema mbali na Chalie Adam pia Spurs walikua wametuma ofa ya kutaka kumsajili mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Italia na klabu ya Villarreal ya nchini Hispania Giuseppe Rossi.

Amesema usiku wa kuamkia jana alikua na matumaini makubwa ya kukamilishwa kwa usajili wa mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 24 lakini hadi dirisha la usajili linafungwa mishale ya saa sita usiku hakufanikikwa kutokana na baadhi ya taratibu kutokukamilishwa kwa muda muafaka.

Mzee huyo mwenye umri wa miaka 63 pia amethibitisha kwamba alituma ofa nyingine za kutaka kuwasajili wachezaji zaidi ndani ya kikosi chake ambapo miongoni mwao yupo mshambuliaji wa klabu ya Athletic Bilbao ya nchini Hispania Fernando Llorente Torres pamoja na washambuliaji wa klabu ya Atletico Madrid ya nchini Hispania Diego Forlán Corazo pamoja na Sergio Leonel "Kun" Agüero del Castillo.
.


No comments:

Post a Comment