KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, February 2, 2011

TUSIIACHE CHELSEA NAYO IMO !!!!


Mshambulaiji wa kimataifa toka nchini Uingereza Mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Mark Rooney amesema Chelsea ndio klabu pekee yenye uwezo wa kuwasumbua mashetani wekundu katika mbio za kusaka ubingwa msimu huu.

Sababu kubwa iliyotolewa na mshambuliaji huyo ambae jana aliifungia timu yake mabao mawili kati ya matatu mbele ya Aston Villa, imejieleza kwamba Chelsea wana kikosi imara ambacho bado kina kila sababu za kuendelea kuubakisha ubingwa huko Stamford Bridge.

Amesema wengi wameidharau klabu hiyo kufuatia misuko suko ya kupoteza baadhi ya michezo mwishoni mwa mwaka uliopita lakini ukweli ni kwamba klabu hiyo bado ina uwezo mkubwa hivyo hawastahili kuidharau hata kwa nukta.

No comments:

Post a Comment