Baada kushindwa kuisaidia klabu yake kuchomoza na ushindi dhidi ya Liverpool katika mchezo wa jana, mshambuliaji mpya wa klabu ya Chelsea Fernando Jose Torres Sanz ameendelea kuwa gumzo mdomoni mwa meneja wake Carlo Michelangelo Ancelotti.
Mshambuliaji huyo amekua gumzo mara baada ya pambano hilo kumalizika huku meneja wake akiamini kwamba ataendelea kushikamana vyema na wahezaji wenzake klabuni hapo na ushindi utapatikana katika michezo ijayo.
Carlo Michelangelo Ancelotti amesema kiujumla mshambuliaji huyo hakucheza vibaya katika mchezo wa jana, na anaamini hatua hiyo imekua nzuri kwake kuanza na kikosi cha klabu ya Chelsea mbacho kinaendelea kushikilia nafasi ya nne kwa kubaki na point 44.
Amesema Fernando Jose Torres Sanz licha ya kuanza vibaya bado alionyesha umahiri wa kutafuta namna ya kuifunga Liverpool lakini kizuizi kilikua safu ya ulinzi ya wapinzani wao ambayo ilijipanga vyema wakati wote.
Hata hivyo meneja huyo wa kimataifa toka nchini Italia ametetea maamuzi yake ya kumchezesha Fernando Jose Torres Sanz sambamba Didier Drogba huku akimuweka Nicolus Anelka nyuma yao ambapo amesema kwamba katika mchezo dhidi ya Sunderland alijaribu kutumuia mfumo humo huo.
Amesema katika mchezo huo alimchezesha Anelka nyuma ya Didier Drogba na walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao manne kwa mawili, hivyo anaamini kuwaanzisha washambuliaji hao wawili katika mchezo wa jana huku akimtumia mfaransa nyuma yao alikua sahihi.
Katika hatua nyingine Ancelotti ameendelea kuamini bado kikosi chake kina nafasi ya kutetea ubingwa wake msimu huu, kufuatia nafasi ya kipekee iliyojitokeza siku moja kabla ya mchezo wa jana ambapo Man Utd walipoteza mbele ya Wolveshampton Wanderers.
No comments:
Post a Comment