KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, February 7, 2011

Jack Andrew Garry Wilshere


Kiungo wa kimataifa toka nchini Uingereza na klabu ya Arsenal Jack Andrew Garry Wilshere hatoadhibiwa na chama cha soka nchini humo kufuatua ujumbe aliokua ameuandika kwenye mtandao wa Twitter kupitia ukurasa wake mara baada ya mchezo wa mwishoni mwa juma lililopita dhidi ya Newcastle Utd huko St James Park.

Jack Andrew Garry Wilshere hatoadhibiwa na chama hicho baada ya kukosekana kwa ushahidi maalum ambao ungemtia hatiani baada ya kuharakisha kuutoa ujumbe huo ambao ulionwa na watu wachache waliountembelea mtandao wa Twitter, ambapo inadaiwa alimshutumu vikali muamuzi Phil Dowd.

Shutuma hizo zilieleza kwamba muamuzi huyo alikua chanzo cha kikosi cha Arsenal kushindwa kuendeleza wimbi la ushindi katika michezo yake ya ligi kuu baada ya kusimamishwa na Newcastle Utd ambao mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika walikua nyuma kwa idadi ya mabao manne kabla ya kuyarejesha katika kipindi cha pili.

Ujumbe huo uliendelea kueleza wazi kwamba Phil Dowd alionekana dhahiri kuipendelea Newcastle Utd kufuatia kuizawadia penati mbili pamoja na kushindwa kutoa maamuzi ya haki kwa kuwaonyesha kadi nyekundu wachezaji wa timu hiyo ambao walionyesha utovu wa nidhamu wa kukithiri.

Endapo chama cha soka nchini Uingereza kingebahatika kuipata ujumbe huo kwenye mtandao wa Twitter kulikua na kila sababu ya kinda huyo kuadhibiwa.

Tatizo kama hilo limewahi kujitikeza ndani ya majuma matatu manne yaliyopita ambapo kama itakumbukwa vyema winga wa zamani wa klabu ya Liverpool Ryan Babel, aliadhibiwa na FA kwa kutozwa faini ya paund 10,000 kufuatia kumtuhumu muamuzi Howard Webb kuwa ni shabiki namba moja wa klabu ya Manchester United ambapo kwa kuhibitisha hilo alitengeneza picha ambazo zilimuonsha amevaa jezi ya klabu hiyo.


No comments:

Post a Comment