KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, February 7, 2011

James Lee Duncan "Jamie" Carragher AMTAKA KING KUSALIA ANFIELD.



Nahodha msaidizi wa klabu ya Liverpool James Lee Duncan "Jamie" Carragher amsisitiza suala la kumtaka meneja wa klabu hiyo King Kenny Dalglish kuendelea kukinoa kikosi cha The Reds na kuachana na mawazo ya kuondoka mwishoni mwa msimu huu kama mkataba wake unavyoelekeza.

James Lee Duncan "Jamie" Carragher amesisistiza jambo hilo mara baada ya mtanange wa jana uliounguruma jijini London ambapo amesema King Kenny Dalglish bado ni meneja ambae anafaa kukiongoza kikosi cha Liverpool hivyo haoni sababu ya kuondoka kwake mwishoni mwa msimu huu.

Beki huyo ambae jana alikua akirejea kwa mara ya kwanza uwanjani mara baada ya kupona jeraha ya kuvunjika bega mwishoni mwa mwaka jana, aliendelea kubainisha kwamba kwa kipindi kifupi kilichopita toka Dalglish alipokichukua kikosi chao toka kwa Roy Hodgson kumekua na mabadiliko makubwa ya kiutendaji katika benchi ya ufundi pamoja na kwa wachezaji pia.

Alipoulizwa suala hilo King Kenny Dalglish, alijibu yeye kilichompelekea katika kikosi cha kwanza cha Liverpool ni kazi pekee hivyo suala la kuendelea kuwepo kwenye kiti hicho ama kuachia mwishoni mwa msimu huu ni suala lingine hivyo linahitaji muda.

Amesema wengi wanauliza suala hilo kila kukicha lakini wanachotakiwa mashabiki pamoja na wachezaji wa klabu ya Liverpool ni kuwa watulivu na kutazama ni vipi watafikia malengo mwishoni mwa msimu huu.

Dalglish pia amempiga kijembe Carlo Ancelotti kwa kusema kwamba yeye hakuhitaji kufanya usajili katika msimu wa dirisha dogo, lakini alilazimishwa na mtaliano huyo kufanya hivyo baada ya kuondoka kwa Ferdinand Torres ambae amedai alicheza vyema katika mchezo wa jana.

No comments:

Post a Comment