KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, February 8, 2011

Diego NJE MECHI MOJA !!!!!!!!


Siku moja baada ya kutimuliwa kazi kwa aliekua meneja wa klabu ya VFL Wolfsburg ya nchini Ujerumani, Steve McClaren, meneja msaidizi wa klabu hiyo Pierre Michael Littbarski aliepewa jukumu la kukiongoza kikosi ametangaza kumsimamisha kiungo wa kimataifa toka nchini Brazil Diego Ribas da Cunha.

Sababu kubwa ya meneja huyo kumsimamisha Diego Ribas da Cunha ni kuchukizwa na kitendo cha ukosaji wa penati kilichofanywa na kiungo huyo katika mchezo wa ligi uliopita ambapo VFL Wolfsburg walikubali kisago cha bao moja kwa sifuri kutoka kwa Hanover 96.

Amesema Diego Ribas da Cunha hakustahili kupiga mkwaju wa penati katika mchezo huo na kabla ya kufanya hivyo alimpokonya mpira Patrick Helmes ambae ndie mpigaji mahsusi wa adhabu kama hizo zinapojitokeza ambapo hata hivyo alikosa mkwaju huo wa penati kwa kugongesha mwamba wa juu wa goli na kuifanya klabu yake kuzama na kupoteza point tatu muhimu, hatua mbayo pia ilichangia kutimuliwa kazi kwa Steve McClaren ambae anadaiwa alikwenda tofauti na malengo aliyowekewa klabuni hapo.

Akithibitisha taarifa hizo kwenye mkutano na waandishi wa habari Littbarski, ambae alikua mmoja wa wachezaji walioiwezesha Ujerumani kutwaa ubingwa wa dunia mwaka 1990, amesema kiungo huyo mwenye umri wa 25 amemuadhibu kwa kutokucheza mchezo ujao wa ligi dhidi ya Hamburg ambao utachezwa siku ya jumamosi.

No comments:

Post a Comment