Baada ya kutangaza kustahafu soka usiku wa kuamkia jana aliekua beki wa klabu ya Man utd pamoja na timu ya taifa ya nchini Uingereza Gary Alexander Neville, ameendelea kupewa shavu ndani ya klabu hiyo ambayo imemlea toka akiwa na umri mdogo.
Taarifa iliyotolewa na uongozi wa klabu hiyo imeeleza kwamba Gary Alexander Neville mwenye umri wa miaka 35 ataendelea kuwepo klabuni hapo hadi mwishoni mwa msimu huu ambapo atasaidiana na kocha mkuu wa timu ya vijana nje ya mkataba na baada ya hapo atasaini mkataba wa kuendelea kukinoa kikosi hicho.
Gary Alexander Neville pia ameingia mkataba na kampuni ya Sky Sports ambapo atakua akitangaza mpira pale timu ya Man utd itakapokua kwenye uwanja wa nyumbani wa Old Trafford katika michezo ya michuano mbali mbali itakayoonyesha kwenye televisheni na kampuni hiyo.
Mapama hii leo Gary Alexander Neville alihojiwa na televisheni ya klabu ya Man utd na kuulizwa ugumu wa maamuzi aliyotyachukua ya kutangaza kuachana na soka baada ya kuitumikia man utd kwa kipindi cha miaka 19 iliyopita.
Amesema kabla ya kufanya maamuzi hayo na kutanga kwenye vyombo vya habari alifanya mazungumzo na meneja wa klabu ya Man utd Sir Alex Ferguson ambae alimtaka atangaze maamuzi hayo mwishoni mwa msimu huu lakini bado akaona kuna umuhimu wa kufanya hivyo katika kipindi hiki.
No comments:
Post a Comment