Winga wa klabu ya FC Twente ya nchini Uholanzi Nacer Chadli ameipiga kumbo nchi ya Morocco na kuamua kuitumikia timu ya taifa ya Ubelgiji ambayo kati kati ya juma lijalo itakua na mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Finland.
Nacer Chadli ambae ni mzaliwa na nchini Ubelgili lakini ana asili ya nchini Morocco amefikia maaamuzi hayo huku tayari akiwa amshaitumikia timu ya taifa ya Morocco mara mbili mwishoni mwa mwaka jana kwenye michezo ya kimataifa ya kirafiki.
Winga huyo mwenye umri wa miaka 21, amesema kabla ya kufanya maamzui hayo alikaa chini na kocha mkuu wa timu ya taifa ya Ubelgiji Georges Leekens ambae alimuita kikosini siku mbili zilizopita na wamefikia makubaliano, ambayo kwake ameyaona yana faida kubwa kuliko kurejea barani Afrika kuichezea timu ya taifa ya Morocco.
Hata hivyo Nacer Chadli alikua ameshaitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Morocco ambacho mwanzoni mwa juma lijalo kitaanza maandalizi ya kujiwinda na mchezo wa kirafiki dhidi ya timu ya taifa ya Niger.
Chadli amebadili mtazamo wa kuichezea timu ya taifa ya Morocco huku zikiwa zimepita siku sita baada ya taifa hilo kutangazwa kuwa mwenyeji wa fainali za mataifa ya bara la Afrika kwa mwaka 2015.
No comments:
Post a Comment