Kipa wa kimataifa toka nchini Hispania pamoja na klabu ya Liverpool José Manuel "Pepe" Reina Páez amemtetea mshambuliaji wa klabu ya Chelsea alieondoka Anfield juma lililopita Fernando José Torres Sanz.
Utetezi wa kipa huyo kwa Torres umeelekezwa kwa mashabiki wa klabu ya Liverpool ambao wanamtuhumu mshambuliaji huyo kwa kumuelezea kuwa msalitui na wala hafai hata kidogo kutazamwa mara mbili akiwa amevaa jezi ya klabu yake mpya ya Chelsea.
José Manuel "Pepe" Reina Páez amesema mshambuliaji huyo alikua hana namna ya kwenda kinyume na matakwa yake ya kuondoka Anfield hivyo anastahili kusamehewa na mashabiki wa klabu ya Liverpool ambao amesema walimpenda na kumthamini wakati wote akiwa klabuni hapo.
Pia amewataka kufikiria namna ya kukisaidia kikosi chao katika kipindi hiki kigumu cha ushindani na kufuta kabisa mawazo ya kuondoka kwa mshambuliaji huyo ambae mwishoni mwa juma lililopita alionja joto ya jiwe baada ya kuanza vibaya akiwa na klabu ya Chelsea kufuatia kisago cha bao moja kwa sifuri kilichotolewa na Liverpool.
No comments:
Post a Comment