Meneja wa klabu ya Man City Roberto Mancini amerejea kauli yake ya kuwataka wachezaji wa klabu hiyo kukaza buti wanapokua uwanjani hasa katika kipindi hiki cha ushindani ambacho kitaamua nani ataibuka kuwa kinara wa ligi kuu ya soka nchini Uingereza.
Mancini ametoa wito huo kwa mara nyingine tena baada ya matokeo ya sare ya mabao mawili kwa mawili yaliyopatikana kwenye mchezo wa jana dhidi ya Birmingham City waliokua nyumbani huko St Andrews Stadium.
Mancini amesema endapo wachezaji wa kikosi chake wataonyesha kubweteka na matokeo yanayopatikana kabla ya kipyenga cha mwisho hakijaopulizwa, kutakua hakuna mafanikio yoyote yanayokusudiwa huko City of Manchester.
Amesema tayari ameshawaeleza wachezaji wake kwamba endapo wanahitaji kupata matokeo mazuri, wanastahili kuachana na kasumba ya kuridhika mapema na badala yake wanastahili kucheza kwa ari hadi dakika ya mwisho.
Wito huo wa Mancini kwa wachezaji wake ameutoa baada ya kikosi chake kuwa mbele kwa idadi ya mabao mawili kwa moja, lakini harakati za kulinda mabao hayo zilishindikana na kujikuta wapinzani wao Birmingham City wakisawazisha kwa mkwaju wa penati uliosababishwa na kiungo wa kimataifa toka nchini Ufaransa Patrick Vieira.
Katika hatua nyingine meneja huyo wa kimataifa toka nchini Italia ameelezea masikitiko yake kufuatia maamuzi ya muamuzi Kevin Friend ya kutoa panati katika amzingira ya kutatanisha.
No comments:
Post a Comment