KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, February 9, 2011

Johan Danon Djourou-Badjere KUWAVAA BARACELONA.


Benchi la ufundi la jeshi la Ashburton Grove, Arsenal hii leo limepokea taarifa njema kutoka nchini Uswiz ambazo zimepunguza hofu ya kumkosa beki wa kimataifa toka nchini humo Johan Danon Djourou-Badjere ambae alizua hofu hiyo baada ya kuumia goti mwishoni mwa juma lililopita katika mchezo wa ligi dhidi ya Newcastle Utd.

Taarifa njema za beki huyo zimetumwa jijini London na mtaalam wa matatizo ya magoti Cuno Wetzel ambae amekua akimtibu beki huyo mara kwa mara pindi anakupata na matatizo hayo.

Amesema beki huyo mwenye umri wa miaka 24, amebainika hakuumia sana sehemu za goti la mguu wake wa kulia zaidi ya maumivu yanayomsumbua hivyo ana uwezo wa kucheza katika mchezo wa ligi ya mabingwa barani ulaya dhidi ya mabingwa wa soka nchini Hispania Fc Barcelona mnamo Februari 16.

Hata hivyo mtaalaamu huyo amelishauri benchi la ufundi la klabu ya Arsenal, kutomtumia Johan Danon Djourou-Badjere katika mchezo wa mwishoni mwa juma hili dhidi ya Wolves ambao wataifunga safari hadi huko Emirates kucheza mchezo wa ligi baada ya kuisimamisha Man utd mwishoni mwa juma lililopita.

Kuumiwa kwa beki huyo kulizua hofu kubwa huko Emirates ambapo kikosi cha meneja Arsene Ernest Charles Wenger kilisaliwa na mabeki wawili wa kati ambao ni Laurent Koscielny pamoja na Sebastien Squillaci huku beki mwingine anaecheza nafasi hiyo Thomas Vermaelen akiendelea kuuguza jeraha la kisigino linalomsumbua toka mwishoni mwa mwezi Septemba mwaka jana.

No comments:

Post a Comment