KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Wednesday, February 9, 2011

NEWCASTEL UTD KUSAJILI WAPYA.



Baada ya kufanikiwa kumuuza mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Uingereza Andrew Thomas "Andy" Carroll, alisajiliwa na klabu ya Liverpool katika msimu wa dirisha dogo mwezi januari, uongozi wa klabu ya Newcastle United umetangaza kutumia fedha kumsajili mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Arsenal Jeremie Aliadiere pamoja na winga wa kimataifa toka nchini Brazil alieachwa na klabu ya Palmeiras Ewerthon Henrique de Souza.

Taarifa kutoka ndani ya klabu hiyo ya St James Park, zinaeleza kwamba tayari bosi mkubwa Mike Ashley ameshampa Baraka zote meneja wa kikoai chake Alan Pardew, kufanya namna yoyote anayoifahamu kwa lengo la kuharakisha anaziba nafasi zilizowazi klabuni hapo ambapo hata hivyo tayari meneja huyo ameshawasilisha orodha ya majina hayo mawili kwa ajili ya kuwezeshwa kwa kila hali.

Katika orodha iliyowasilishwa mezani kwa Mike Ashley imeonyesha kwamba sababu kubwa ya kutaka kusajili kwa Jeremie Aliadiere ambae ni raia wa nchini Ufaransa ni kufuatia kuwa huru kwa sasa baada ya mkataba wake na klabu ya Middlesbrough kufikia kikomo mwishoni mwa msimu uliopita hivyo anaweza kujunga na klabu yoyote kwa hivi sasa.

Mshambuliaji huyo kwa sasa anaripotiwa kufanya mazoezi na vikosi vya baadhi ya vilabu vya sokla huko nchini kwao Ufaransa kwa lengo la kujiweka fit.

Kwa upande wa Ewerthon Henrique de Souza, nae imeelezwa yu huru kwa sasa baada ya uongozi wa klabu yake ya Palmeiras kumuacha katika kipindi cha usajili cha mwezi Januari hivyo nae ana nafasi kubwa ya kujiunga na klabu ya Newcastle Utd wakati wowote kuanzia hivi sasa.

Wakala wa winga huyu mwenye umri wa miaka 29, Barry McIntosh alipoulizwa juu ya suala la mchezaji wake kuwa mbioni kuelekea barani Ulaya, alikubaliana na suala hilo ambapo amesema katika kipindi cha siku mbili tatu zilizopita amekua na mazungumzo na viongozi wa klabu ya Newcastle Utd.

No comments:

Post a Comment