Kipa wa kimataifa toka nchini Poland pamoja na klabu ya Arsenal Lukasz Fabianski atalazimika kuwa nje ywa uwanja kwa kipindi cha msimu kilichosalia kufuatia kuumia bega majuma kadhaa sasa.
Taarifa za kuwa nje kwa kipa huyo mwenye umri wa miaka 25, zimetolewa hii leo na meneja wa klabu ya Arsenal Arsene Wenger alipokutana na waandishi wa habari kuzungumzia mchezo wa mwishoni mwa juma hili ambapo kikosi chake kitafunga safari hadi huko St James Park kucheza na wenyeji wao Newcastle Utd.
Wenger amesema Lukasz Fabianski anatarajia kufanyiwa upasuaji wa bega siku kadhaa zijazo huko nchini Ujerumani.
Lukasz Fabianski kwa kipindi cha majuma manne sasa amekua haonekana kwenye kikosi cha kwanza cha Arsenal ambapo kwa mara ya mwisho alijumuishwa kikosini kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Manchester City mnamo Januari 05.
Hata hivyo Arsene Wenger amesisitiza kwamba, kuwa nje kwa kipa huyo bado kutaendelea kumap nafasi kipa chaguo la tatu Wojciech Szczesny ambae amekua mbadala klabuni hapo toka alipoanza kuonekana kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Man utd.
Wenger amesema nafasi kwa kipa wa kimataifa toka nchini Hispania Manuel Almunia kurejea katika kikosi cha kwanza bado ni hafifu kufuatia kuhitaji maandalizi ya kutosha baada ya kuwa nje kwa kipindi cha miezi minne iliyopita kabla ya kurejea tena uwanjani mwishoni mwa juma lililopita kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya Huddersfield Town.
No comments:
Post a Comment