KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, February 4, 2011

King Kenny Dalglish AKIRI KUUMIZWA NA SAFARI YA TORRES.



Meneja wa sasa wa klabu ya Liverpool King Kenny Dalglish amekiri kusikitishwa na harakati za kuondka kwa mshambuliaji huyo na kujiunga na klabu ya Chelsea.

Kin Kinny ametoa kauli ya kusikitishwa na hatua hiyo ikiwa ni baada ya siku tatu kupita ambapo aliwataka mashabiki na wachezaji wa klabu ya Liverpool kusahau yaliyopita na kufungua ukurasa mpya ambao utawasababishia kumsau Torres.

Amesema licha ya yeye kusikitishwa na hatua ya kuondoka kwa mshambuliaji huyo aliedumu huko Anfield kwa muda wa miaka mitatu kuanzia mwaka 2007-2011, pia viongozi wa ngazi za juu wamesikitishwa na hatua hiyo lakini bado akaendelea kutoa msisitizo wa kumtaka kila mmoja wao kusahau yaliyopita.

Wakati Dalglish akizungumza kwa uchungu juu ya kuondoka kwa Ferdinand Torres aliejiunga na klabu ya Chelsea usiku wa kuamkia Februari Mossi, mshambulaiji mpya wa klabu ya Liverpool Andrew Thomas Carroll *Andy Carroll* amemliwaza meneja wake kwa kuahidi kufanya kila kinachowezekana kwa ajili ya kuiwezesha The Reds kufikia malengo yake msimu huu.

Andy Carroll ametoa ahadi hiyo alipokua akitambulishwa kwa waandishi wa habari usiku wa kuamkia hii leo ambapo amesema anafahamu kwa sasa kinachomkabilio ni kurejesha fadhila za uongozi wa klabu yake mpya ambao wametumia kiasi kikubwa cha fedha kumsajili klabuni hapo.

Amesema alishangazwa na ada ya uhamisho wake iliyolipwa kwenye klabu yake ya zamani ya Newcastle Utd ambayo imemfanya kuwa mchezaji wa kiingereza aliesajiliwa kwa kiasi kikubwa cha fedha.

Katika hatua nyingine mshambulaiji huyo mwenye umri wa miaka 22 amekataa kata kata kuzungumzia suala la klabu yake ya zamani huku akiwataka waandishi wa habari kumuuliza juu ya klabu yake mpya ya Liverpool.

No comments:

Post a Comment