KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Friday, February 4, 2011

SITISHANGILIA NIKIWAFUNGA LIVERPOOL.


Fernando Torres amesema daima ataiheshimu Liverpool na kuipenda, na katu hatorejesha maneno wala vitendo atakavyo onyeshwa na mashabiki wa klabu hiyo popote pale atakapokutana nao hapa ulimwenguni.

Torres asema Liverpool ni klabu kubwa kwake na imempa heshima dunia hivyo atakua mpuuzi na mjinga endapo atakwenda kinyume na utaratibu wa maisha yake aliojiwekea toka alipojiunga na The Reds waliomsajili mwaka 2007 akitokea nyumbani kwao Hispania katika klabu ya Atletico Madrid.

Amesema hata kamna itatokea akifunga bao katika mchezo wa siku ya jumapili dhidi ya Liverpool hatoshangilia kwani anajua ni vipi atakavyoumia moyoni.

No comments:

Post a Comment