Uhamisho ulioweka rekodi huko nchini Uingereza wa paund million 50 uliozihusishwa klabu za Chelsea pamoja na Liverpool kupitia kwa mashambuliaji wa kimataifa toka nchini Hispania Fernando José Torres Sanz umeendelea kuwa gumzo.
Usajili huo uliochukua nafasi siku ya mwisho ya msimu wa usajili wa dirisha dogo kwa kushuhudia mshambuliaji huyo akitoka Anfied na kuelekea Stamford Bridge, hii leo umezungumzia na aliekua meneja wa klabu ya Liverpool Rafael Benítez ambapo amesema usajili huo ulistahili kuvunja rekodi siku nyingi zilizopita.
Rafael Benítez amesema wakati akiwa meneja wa klabu hiyo ya mjini Liverpool, uongozi wa klabu ya Chelsea ulionyesha dhamira ya kuhitaji kumsajili mshambuliaji huyo na yeye aliwaeleza wazi kwamba Torres hawezi kuondoka kwenye himaya ya Anfield hadi itakapotolewa ada ya uhamisho wa paund million 70.
Katika hatua nyingine meneja huyo wa kimataifa toka nchini Hispania ambae alifungashiwa virago huko Inter Milan nchini Italia, mwishoni mwa mwaka 2010, amekiri kuitamani klabu ya Liverpool lakini akabainisha wazi kwamba kwa sasa tamaa yake haiwezi kumalizwa kutokana na uwepo wa King Kenny Daldlish.
Hata hivyo Benitez amesema bado ana ndoto za kurejea tena klabuni hapo siku za usoni kukinoa kikosi cha klabu ya Liverpool ambacho alikua nacho kwa kipindi cha miaka sita kuanzia mwaka 2004–2010.
No comments:
Post a Comment