KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, July 16, 2009

BADO TERRY SASA !!!!!!!!!!!!!!!!???????

MARK HUGHES amemuomba John Terry kuhakikisha anaipa mgongo klabu yake ya Chelsea kwa lengo la kuongeza hatua ya kufanya mapinduzi ndani ya klabu ya Manchester City.

Boss huyo wa Man City amesema umewadia wakati kwa beki huyo wa kimataifa toka nchini Uingereza mwenye umri wa miaka 28 kubadilisha muelekeo wake wa kucheza soka katika mazingira mapya.

Hughes amesema kutokana na uzoefu wa beki huyo ambae ameichezea klabu yake ya Chelsea kwa muda mrefu anatakiwa kukabiliana na changamoto nyingine ili aweze kuendelea kutimiza ndoto zake.

Amesema lengo lake si kumshawishi Terry kwa sababu ya fedha bali anataka mchezaji huyo kujenga hatua ya kukabiliana na changamoto ambazo zinaweza kubadilisha muelekeo wake katika mafanikio ya hii leo na hapo baadae.

Hughes aliewahi kuuona uwezo wa Terry alipokuwa anaichezea klabu ya Chelsea kati ya mwaka 1995 na 1998 amesema mchezaji huyo ana uwezo mkubwa wa kuwa kiongozi kwa maana ya unahodha.

Meneja huyo ameongeza kuwa anaamini hatua ya kusajiliwa kwa mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Argentina Carlos Tevez kutawahamasisha wachezaji wengine nyota ulimwengini kujiunga na klabu hiyo.

No comments:

Post a Comment