KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Thursday, July 16, 2009

NJIA NYEUPE KWA ADEBAYOR.

Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Togo Emmanuel Adebayor amefanikiwa kupimwa afya yake na anataraji kujiunga na klabu ya Manchester City baada ya kibali cha kufanyika kazi ndani ya klabu hiyo kuhakikiwa.

Adebayor anatarajiwa kuelekea City Of Manchester akitokea kwenye klabu ya ya Arsenal aliyoichezea kwa muda wa miaka mitatu na nusu ambayo imekubalidi dili la paund milion 25 kama ada ya uhamisho wake.

Mbali na klabu ya Manchester City kuonekana kufanikiwa kumsajili mshambuliaji huyo alieifungia The Gunners mabao 16 msimu uliopita vile vile Adebayor alikuwa akihusishwa na taarifa za kutaka kusajiliwa na klabu za AC Milan na Chelsea.
Katika hatua nyingine meneja wa klabu ya Manchester City Mark Hughes amesema bado klabu hiyo itaendelea kuwasajili wachezaji nyota kwa ajili ya kukijenga kikosi chake msimu ujao.

Akiongea na waandishi wa habari kuthibitisha kumsajili aliyekuwa mshambuliaji wa klabu ya Manchester Uinted Carlos Tevez, meneja huyo amesema bado klabu hiyo inahitaji wachezaji katika nafasi kadhaa kabla ya kuhitimisha lengo lake la usajili.

Manchester City ina lengo la kuwa miongoni mwa klabu zilizo na vikosi bora msimu ujao hatua ambayo imedhihirika kufuatia klabu hiyo kutumia kiasi kikubwa cha fedha katika usajili.

Iwapo klabu hiyo itakamilisha usajili wa Adebayor itakuwa imefanikiwa kuwasajili wachezaji kutoka klabu tatu kati ya sita zilizokuwa katika nafasi za juu msimu uliopita.


No comments:

Post a Comment