KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Tuesday, July 14, 2009

CARLO ANCELOTTI AANZA KUUNGURUMA.


MENEJA wa klabu ya Chelsea CARLO ANCELOTTI anaamini yeye kama mmoja wa viungo bora aliyefanikiwa kutwaa medali katika michuano ya klabu bingwa barani ulaya atapewa heshima ya kutosha na wachezaji wa klabu yake mpya.

Angalizo hilo limekuja ili kuwataka wachezaji wake wajue aina ya uongozi atakaoutumia wakati anatekeleza wajibu wake na kuongeza kuwa anapenda kuwaona wachezaji wanakuwa na bidii mazoezini.

Ancelotti amesema wakati anachezaji soka hakuwa mchezaji mkimya bali alikuwa na bidii uwanjani na hakupenda kushindwa na mchezaji yoyote wa timu pinzani hivyo angependa wachezaji wa klabu hiyo wamuheshimu kama meneja wao.

Amesema atakuwa mwamuzi katika masuala ya kiufundi lakini pia atawaheshimu wachezaji wake atakaofanya nao kazi ili kujenga mahusiano mazuri.


Amesema lengo lake ni kuwa na wachezaji watakaokuwa na uweza kucheza vizuri kwa kipindi kirefu klabuni hapo.

Kuhusu utovu wa nidhamu ulioonyeshwa na mshambuliaji Didier Drogba aliyefungiwa kucheza michezo minne katika michuano ya kombe la mabingwa msimu ujao , Ancelotti amesema anafahamu hali aliyokuwa nayo mshambuliaji huyo jambo ambalo linaweza kumtokea mchezaji yoyote anaehisi kuonewa.

Wakati huohuo ancelotti anakabiliwa na kibarua kigumu cha kumshawishi nahodha wa klabu hiyo John Terry kuendelea kubaki Stamford Bridge baada ya kuwepo taarifa za kutaka kusajili na klabu ya Manchester City.


Mwishoni mwa juma lililopita wawakilishi wa Terry alikutana na mmiliki wa klabu hiyo Roman Abramovich na kuzungumza hatma ya mchezaji huyo kuendelea kubaki Chelsea.
Katika hatua nyingine mlinda mlango wa klabu hiyo PETR CECH ameshauriwa na madkari kuendelea kuvaa kinga kichwani.

Chech amesema madaktari wameshauri kuendelea kuwa na kinga baada ya kukiri kwamba bado hajapona vizuri.
Itakumbukwa kwamba kipa huyo wa Chelsea alipata mpasuko katika fuvu lake mnamo mwaka 2006 alipokuwa kwenye purukushani za kudaka mpira mbele ya mshambuliaji wa klabu ya Reading Stephen Hunt aliemgonga na goti.



No comments:

Post a Comment