MLINDA mlango wa klabu ya Arsenal MANUEL ALMUNIA amesisitiza kwamba atafurahi kama ataitwa kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Uingereza.Almunia ametimiza vigezo vyote vya kuichezea timu hiyo ya taifa ua Uingereza kutokana na kuwa na nafasi ya kupata hati ya kusafiria ya Uingereza ambapo fursa hiyo imekuja baada ya kuichezea klabu ya Arsenal kwa muda wa miaka mitano.
Kipa huyo mwenye umri wa miaka 32 amesisitiza kuwa itakuwa vigumu kwake kuitwa katika timu ya taifa ya Hispania baada ya kuzaliwa na kukuliwa nchini Uingereza hivyo itakuwa ni heshima kwake kuvaa jezi zenye alama ya simba watatu kifuani akimaanisha timu ya taifa ya Uingereza.
Iwapo ataitwa katika kikosi hicho anataraji kukutana na upinzani mkubwa kutoka kwa makipa wenzake David James, Rob Green, Ben Foster, Scott Carson na Paul Robinson wanaotaka nafasi ya kuwemo kwenye kikosi kitakachoshiriki fainali za kombe la Dunia mwaka 2010 nchini Afrika Kusini iwapo Uingereza itafuzu.
No comments:
Post a Comment