
Mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Uholanzi na klabu ya Real Madrid Klaas-Jan Huntelaar amekubali kujiunga na klabu ya Stuttgart ya nchini Ujerumani.
Klabu ya Stuttgart imekamilisha utaratibu huo wa usajili wa mchezaji huyo kwa lengo la kuziba mwanya ulioachwa wazi na mshambuliaji wao wa kimataifa toka nchini ujerumani Mario Gomez ambae amejiunga na klabu ya Bayern Munich kwa ada ya uhamisho wa paund million 20.
Mshambuliaji huyo anaondoka huko St Bernabeu, baada ya kuwekwa kwenye orodha ya wachezaji ambao wanatakikana kuuzwa katika kipindi hiki cha usajili kufuatia hatua za kusajili kwa wachezaji wengine klabuni hapo.
Miongoni mwa wachezaji ambao wametoa changamoto kwa Huntelaar kuondoka Real Madrid ni pamoja na Kaka, Cristiano Ronaldo pamoja na Karim Benzema.
Kukubali huko kwa Klaas-Jan Huntelaar kunamaliza uvumi wa klabu za nchini Uingereza zilizokuwa zinamuhitaji kwa udi na uvumba ikiwemo klabu ya Arsenal pamoja na Manchester City ambayo hata hivyo mwishoni mwa juma lililopita ilifanikiwa kumnasa mshambuliaji Emmanuel Adebayor.
Klabu nyingine ya nchini Uingereza iliyokuwa ikimuhitaji Klaas-Jan Huntelaar ni Tottenham ambayo ilionekana kupania kukamilisha uhamisho wake lakini ilishindwa kufikia malengo hayo baada ya kuvunjika kwa mazungumzo yaliyokuwa yanaendelea kati yao na uongozi wa klabu ya Real Madrid.
No comments:
Post a Comment