KARIBU KWENYE BLOGU YA XTRA COVER ILI UWEZE KUFAHAMU YALE YANAYOTOKEA NJE YA MIPAKA YA NCHI YETU, PIA WAWEZA KUTOA MAONI YAKO KWA TAARIFA YOYOTE ITAKAYO KUKUNA.

Monday, July 20, 2009

LIVERPOOL WACHEMSHA KWA RAPID VIENA.

Steffen Hofmann


Klabu ya Liverpool usiku wa kumakia leo ilishindwa kufurukuta mbele ya klabu ya Rapid Vienna ya nchini Austria baada ya kuchapwa bao moja kwa sifuri.

Mchezo huo ambao ni wa kirafiki na wenye lengo la kuizandaa klabu hizo na msimu mpya wa ligi wa mwaka 2009-10 ulishiudia Liverpool wakipachikwa bao hilo na mshambuliaji wa Rapid Vienna Steffen Hofmann katika dakika ya 57.

Katika kipindi cha kwanza Rapid walipata bao kupitia kwa Erwin Hoffer ambapo hata hivyo bao hilo lilikataliwa na mwamuzi kwa madai ya kuwa mchezaji huyo alikuwa ameotea kabla ya kuukwamisha mpira nyavuni.

Hata hivyo Liverpool ilikuwa imesheheni wachezaji wake mahiri kama Steven Gerrard, Jamie Carragher pamoja na Yossi Benayoun.

Gerrard pamoja na Carragher walicheza katika kipindi cha kwanza huku Benayoun pamoja na mshambuliaji wa kimataifa toka nchini Uholanzi Dirk Kuyt wakicheza katika kipindi cha pili kufuatia mabadiliko yaliyofanywa na meneja wao Rafael Benitez.

Beki wa kimataifa toka nchini Uingereza Glen Johnson ambae amesajiliwa na klabu hiyo kwa ajili ya msimu mpya wa ligi hapo jana alipumzishwa kufuatia kuykabiliwa na maumivu ya kifundo cha mguu aliyoyapata kwenye mchezo wa kati kati ya juma lililopita dhidi ya St Gallen.

No comments:

Post a Comment